1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yataka kufungwa shirika la wakimbizi Palestina

Sekione Kitojo
8 Januari 2018

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa mwito wa kufungwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina, siku kadhaa baada ya rais Donald Trump kutishia kupunguza misaada kwa Wapalestina.

https://p.dw.com/p/2qUNS
Belgien Brüssel Netanjahu trifft Mogherini
Picha: Reuters/F. Lenoir

Israel pia imeyataja makundi 20 ya wanaharakati duniani kote ambao wanachama wake watapigwa marufuku kuingia nchini humo kuhusiana na miito yao ya kulisusia  taifa la  Kiyahudi.

Israel kwa muda mrefu inaliona shirika hilo la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina, lijulikanalo kama UNRWA kuwa lina upendeleo dhidi ya nchi hiyo, madai yanayokanushwa vikali na shirika hili, likisema linatoa tu huduma muhimu kwa Wapalestina, UNRWA ni shirika linaloendeleza matatizo ya wakimbizi wa Wapalestina, amesema Netanyahu wakati huohuo akimsifu rais Trump mwanzoni mwa kikao cha baraza la mawaziri cha kila wiki.

Israel Netanyahu - Kabinettssitzung
Kikao cha baraza la mawaziri la Israel Picha: Reuters/D. Bality

Amesema  wakati  mamilioni  ya  wakimbizi  wengine duniani  kote  wanapatiwa  huduma na shirika  la  Umoja wa  mataifa  la  kuwahudumia  wakimbizi  UNHCR , Wapalestina  wana  shirika  lao ambalo pia  linawahudumia "wajukuu  wa  wakimbizi  ambao  kwa  mtazamo  wake  si wakimbizi.

Hali  hii  isiyoeleweka  ni  lazima  ifikie  mwisho," Netanyahu alisema.

Kauli ya Netanyahu yapingwa

"Pendekezo  langu  liko  wazi , kuipatia  fedha  UNRWA ni lazima kuhamishiwe  taratibu  katika  shirika  la Umoja wa Mataifa  la  kuwahudumia wakimbizi UNHCR , kwa utaratibu maalum  wa  kusaidia wakimbizi  wa  kweli na  sio  wale ambao  si wa  kweli, kama  inavyotokea  leo  chini  ya UNRWA."

Msemaji  wa  UNRWA  Chris Gunness  amesema  kwamba mamlaka  ya shirika  hilo  yametolewa  na  baraza  kuu  la Umoja  wa  Mataifa, ambalo  wanachama  wake  wanatoa uungaji  mkono  mkubwa  kwa shirika  hilo  la  kutoa misaada  ya maendeleo na kiutu". 

"Kile  kinachoendeleza  mzozo  wa  wakimbizi ni  kushindwa kwa  pande  hizo kushughulikia suala  lenyewe,"  aliandika katika  taarifa.

"Hali  hii inapaswa  kutatuliwa  na  pande  zinazohusika  na mzozo  huo  katika muktadha  wa  mazungumzo  ya amani, yaliyo chini  ya  maazimio  ya  Umoja  wa  mataifa na  sheria  za  kimataifa,"  amesema  Chris Gunness.

IS-Kämpfer verlassen Palästinenserlager Jarmuk in Damaskus
Wakimbizi wa Kipalestina katika kambi ya Jarmuk mjini Damascus Syria ambao shirika la UNRWA linawahudumiaPicha: picture-alliance/AP Photo/UNRWA

Mwezi  Juni , Netanyahu  alisema  alilizungumza  suala hilo pamoja  na  balozi  wa  Marekani  katika  Umoja  wa Mataifa Nikki  Haley.

Wanaharakati kupigwa marufuku

Wakati  huo  huo  Israel  mwaka  jana  ilipitisha  sheria ambayo  itapiga  marufuku mwanaharakati  yeyote  ambaye "kwa  makusudi  kabisa  anatoa  wito  wa  kuisusia Israel." Orodha  iliyotolewa  jana  Jumapili, ambayo  inajumuisha shirika  lililotuzwa  nishani  ya  amani  ya  Nobel , inaambatana  na  sheria  hiyo.

"Mashirika  yanayotaka  Israel  itengwe yanapaswa kutambua  kwamba  taifa  la  Israel litachukua  hatua dhidi yao,"  amesema  waziri  wa  mikakati  Gilad Erdan  katika taarifa.  Orodha  ya makundi  hayo  ni  kutoka  Marekani, Ufaransa, Afrika  kusini  na  kwingineko.

Kamati  ya Marafiki  wa  Marekani  wa  kutoa  huduma , kundi  ambalo  limo  katika  orodha  hiyo , limesema litaendelea  kufanyakazi  kwa  ajili  ya "amani  na  haki." Kundi  hilo  pamoja  na  shirika  la  Quaker  la  Uingereza yalishinda  tuzo  ya  amani  ya  Nobel  mwaka  1947 kwa kuwasaidia  wakimbizi  wa  vita  vikuu  vya  dunia.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / ape / afpe

Mhariri: