Israel yashinikizwa kuchukua hatua zaidi kuokoa mateka
4 Februari 2024Matangazo
Maandamano hayo yaliofanyika katika miji kadhaa ya Israel ikiwemu mji wa pwani wa Tel Aviv na Jerusalem yamewahusisha wanafamilia wa mateka yakiwa na kauli mbiu "siku 120 chini ya ardhi."
Katika maeneo mengine waandamanji walimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu kwa kile walichokitaja kutochukua juhudi zaidi ili kuachiliwa kwa mateka.
Soma pia:Netanyahu: Sitaridhia makubaliano ya kusitisha mapigano
Vyama vya mrengo wa kulia Israel vimetishia kuvunja muungano unaotawala ikiwa Netamyahu atafanya makubaliano na Hamas.
Inaripotiwa wapatanishi wa Israel wamekubali pendekezo la kusitisha mapigano na kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina, pendekezo ambalo linatoa nafasi ya kuachuliwa huru kwa mateka, na sasa Hamas inasubiriwa kuidhinisha.