1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia makao ya Umoja wa Mataifa Lebanon

10 Oktoba 2024

Kifaru cha jeshi la Israel kimeshambulia makao makuu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon na kujeruhi wafanyikazi wawili.

https://p.dw.com/p/4ldyj
Libanon-Israel-Konflikt Hisbollah | UN-Soldat an Grenze
Picha: Daniel Carde/Getty Images

Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) kimesema kifaru cha jeshi la Israel kilenga moja kwa moja kituo cha ufuatiliaji cha Umoja wa Mataifa katika eneo dogo la mji wa Naqoura.

Hata hivyo jeshi la Israel halijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulizi hilo.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifuatilia eneo la mpaka kati ya Lebanon na Israeli kwa miongo kadhaa ukiwa na zaidi ya wanajeshi 10,000 kutoka mataifa 50 wengi wao wakitokea Indonesia, Italia na India.