1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yasema uwezekano wa makubaliano na Hezbollah ni finyu

16 Septemba 2024

Israel yaonya juu ya kufifia uwezekano wa makubaliano ya kusitisha vita na Hezbollah.

https://p.dw.com/p/4kgmi
USA Verteidigungsminister Austin empfängt den israelischen Verteidigungsminister Gallant im Pentagon
Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant akiwa na mwenzake wa Marekani Lloyd Austin katika PentagonPicha: Michael Reynolds/EPA


Waziri wa ulinzi wa Israel ameiambia Marekani kwamba uwezekano wa kusitishwa vita na kundi la wanamgambo wa Hezbollah katika mpaka wa Lebanon, unazidi kutoweka.

Yoav Gallant amemwambia mwenzake wa Marekani, Lloyd Austin katika mazungumzo yao ya simu kwamba uwezekano wa kufikiwa makubaliano upande wa Kaskazini na Lebanon unafifia kwasababu kundi la Hezbollah linaendelea kujifungamanisha na Hamas.

Soma pia: Israel yaendelea kukabiliana na Hezbollah

Kundi hilo la Hezbollah limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Israel kila siku tangu wanamgambo wa Hezbollah walipoivamia Israel Octoba 7.

Naibu wa kundi hilo Naim Qassem Jumamosi alisema Hezbollah halina nia ya kuingia vitani lakini ikiwa Israel itaanzisha vita,pande zote zitaathirika.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW