Israel yajiandaa kuwapokea mateka watakaoachiliwa na Hamas
24 Novemba 2023Hayo yamewezeshwa chini yamakubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa leo yanayojumuisha pia uwasilishwaji wa misaada ya kiutu na mafuta huko Gaza.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ambaye nchi yake imesaidia katika kufikiwa kwa makubaliano hayo amesema mpango huu wa kusitisha mapigano kwa siku nne na kutanuliwa mpango huo ili mateka zaidi wanaoshikiliwa na Hamas waweze kuachiliwa huru na pia kuruhusu misaada ambao utawasaidia watu milioni 2.3 ambao wana mahitaji makubwa kuanzia maji, chakula, msaada wa matibabu na kila kitu.
Wakati huo huo Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema mpango huo wa usitishwaji mapigano huko Gaza ni wa muda mfupi tu, na kwamba baadaye nchi yake itaendeleza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas.