Israel yaishambulia tena Lebanon
26 Februari 2024Matangazo
Shambulizi hilo ni la kwanza la aina hiyo mashariki mwa Lebanon tangu kuanza kwa uhasama kati ya Israel na kundi hilo baada ya kuzuka kwa vita katika Ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israel limesema mashambulizi hayo yalilenga mifumo ya ulinzi ya anga ya Hezbollah kulipiza kisasi dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran kwa kuiangusha droni yake moja kusini mwa Lebanon mapema leo.
Chanzo kimoja cha Hizbullah kimethibitisha idadi hiyo ya vifo.
Chanzo kingine kimesema kuwa mashambulizi ya Israel yalilenga jengo linalotumiwa na Hizbollah katika kitongoji hicho cha Baalbek.
Vyanzo vyote viwili vilizungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kukosa idhini ya kuzungumza na waandishi habari.