1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza

24 Desemba 2023

Israel imeendeleza mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza, huku kundi la Hamas likiripoti hujuma kubwa katika miji kadhaa saa chache baada ya mataifa yenye nguvu duniani kutaka msaada zaidi uruhusiwe katika eneo hilo

https://p.dw.com/p/4aWRn
Moshi unaotokana na mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza kwenye mapigano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kundi la Hamas
Moshi unaotokana na mashambulizi ya Israel katika ukanda wa GazaPicha: Ronen Zvulun/REUTERS

Wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas,  imesema watu 18 wameuawa kutokana na nyumba moja kushambuliwa katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza, huku shabaha zingine pia zikilengwa.

Soma pia:Vikosi vya Israel vyaelekeza mashambulizi katikati mwa Gaza

Hapo jana jioni, jeshi la Israel lilisema kuwa limeharibu ''handaki moja la kimkakati'' lililolitaja kuwa ''makao makuu ya Hamas na kuwauwa magaidi'' wakati wa operesheni katika mji wa Gaza City ambapo wanajeshi wake wamekuwa wakikabiliana katika mapigano ya ardhini na wapiganaji wa Hamas.

Soma pia: Azimio kuhusu vita vya Gaza kupigiwa kura

Mapigano yanaendelea hata baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kutaka misaada zaidi ipelekwe kwenye Ukanda wa Gaza haraka.

Azimio hilo lilipitishwa baada ya kuahirishwa mara tatu.