1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendelea kuishambulia Lebanon

30 Septemba 2024

Israel imeendelea na mashambulizi yake ndani ya Lebanon na kwa mujibu wa taarifa, jengo moja la makaazi limeshambuliwa katikati ya mji wa Beirut.

https://p.dw.com/p/4lEKj
Lebanon, Beirut | mashambulizi ya Israel
Mojawapo ya athari za mashambulizi ya Israel nchini Lebanon.Picha: Hassan Ammar/AP/picture alliance

Maafisa wa Lebanon wamesema watu zaidi  ya 100  wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kundi la Hamas limetoa taarifa kwamba kiongozi wao, Fatah Sharif, aliuliwa pamoja na baadhi ya watu wa familia yake kwenye mashambulizi yaliyofanywa na Israel kusini mwa Lebanon.

Soma zaidi: Hezbollah yavurumisha makombora dhidi ya Israel

Na mapema leo kambi ya wakimbizi ya wapalestina iliyopo karibu na mji wa bandari wa Tyre nchini Lebanon pia ilishambuliwa.

Hamas yenye makao yake katika Ukanda wa Gaza limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na serikali ya Ujerumani, Umoja wa Ulaya, Marekani na baadhi ya mataifa ya Kiarabu.

Wakati huo huo, kundi la wanamgambo linaloitwa la kupigania Ukombozi wa Palestina (PFLP), limesema kwenye taarifa kwamba pia wanachama wake kadhaa wameuawa katika shambulio hilo la anga la Israel katika mji wa Beirut, leo Jumatatu.