MigogoroMashariki ya Kati
Israel yaendelea kuishambulia eneo la Bureij Gaza
4 Juni 2024Matangazo
Jeshi la Israel limetangaza pia kuwa mateka wengine wanne waliokuwa wakishikiliwa na Hamas wameripotiwa kufariki.
Umoja wa Mataifa umetaja wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya huko Khan Younis na Deir al-Balah.
Soma pia:Zaidi ya nusu ya miundombinu yote Ukanda wa Gaza imeharibiwa
Hayo yanajiri wakati Marekani imelihimiza hapo jana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono mpango wa awamu tatu uliotangazwa na Rais Joe Biden, ambao unalenga kumaliza vita vya takriban miezi minane huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na kutumwa misaada.