1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel layashambulia maeneo ya Lebanon

23 Septemba 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya na kuyalenga maeneo ya kundi la Hezbollah kusini mwa Lebanon, katika bonde la mashariki la Bekaa na eneo la kaskazini karibu na Syria.

https://p.dw.com/p/4kyJv
Msemaji wa Israel Daniel Hagari
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Israel Daniel Hagari amesema watafanya jitihada za kuwarejesha raia wa Israel walioondoka maeneo yao kutokana na vitaPicha: Gil Cohen-Magen/AFP

Msemaji wa jeshi la Israeli Daniel Hagari amesema watafanya kila kinachohitajika ili kuwarejesha kwenye makaazi yao raia wa kaskazini mwa Israel waliohamishwa. 

Amesema hayo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu uwezekano wa Israel kuendesha operesheni ya ardhini huko Lebanon.

Jeshi la Israel limewatolea wito raia wa kusini mwa Lebanon kuondoka karibu na maeneo yanayotumiwa na Hezbollah kuvurumisha makombora kuelekea Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz amemshutumu kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah kuwatumia raia wa Lebanon kama ngao kwa kuhifadhi silaha na makombora kwenye nyumba zao.