Israel yafanya mashambulizi ya anga ndani ya Lebanon
25 Agosti 2024Kundi la Hezbollah limesema mashambulizi iliyafanya ni kulipiza kisasa cha mauaji ya kamanda wake mkuu.
Jeshi la Israel limesema katika taarifa kwamba, ndege zake za kivita ziliharibu maelfu ya roketizilizokuwa zimeelekezwa na Hezbollah kaskazini na katikati mwa Israel, na zilikuwa zinalenga kushambulia katikati mwa taifa hilo.
Hezbollah imejibu taarifa hiyo ikisema Israel imekuwa ikitoa "madai matupu" ya kuzuia shambulio hilo, na kuongeza kwamba oparesheni yake hiyo ya Jumapili "imekamilika kwa mafanikio."
Soma pia:Kamanda wa Hezbollah auawa katika shambulizi la anga
Hezbollah na Israel zimekuwa zikishambulia karibu kila siku katika kipindi chote cha vita vya Gaza, katika kile inachokisema mashambulizi ya kuunga mkono mshirika wake wa karibu kundi la Kipalestina la Hamas.
Hofu ya kutanuka kwa mzozo huo katika kanda ya Mashariki ya Kati iliongezeka baada ya shambulio la Israel katika mji wa Beirut mnamo mwezi Julai na kumuua kamanda mkuu wa Hezbollah Fuad Shukr na kusababisha nadhiri ya kulipiza kisasi dhidi ya mauaji hayo.