1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel kufungua kwa muda vituo viwili kuingiza misaada Gaza

5 Aprili 2024

Israel imetangaza usiku wa kuamkia leo kuwa itaruhusu "uingizaji wa muda" wa misaada ya kiutu kupitia mpaka wake na kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eRqe
Hali kwenye Ukanda wa Gaza
Mashirika ya kimataifa yanasema Ukanda wa Gaza unakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.Picha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/picture alliance

Taarifa hiyo iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, imesema vituo vya Ashdod na Erez ndiyo vitatumika kupeleka misaada ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.

Tangazo hilo limetolewa muda mfupi baada ya Netanyahu kufanya mazungumzo na rais Joe Biden wa Marekani.

Kwenye mazungumzo hayo ya simu yaliyodumu kwa dakika 30, rais Biden alimtaka Netanyahu kuonesha kwa vitendo kuwa Israel inachukua hatua akionya kuwa Marekani itatafakari upya sera yake kuelekea vita vya Gaza kwa kuzingatia hatua ambazo nchi hiyo itazitekeleza.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili kwa sehemu kubwa yalijikita juu ya shambulio lililofanywa na Israel ambapo liliwaua wafanyakazi 7 wa kutoa misaada ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.

Mkasa ulizusha lawama kubwa kutoka jumuiya ya kimataifa.