Israel imetishia kufanya mashambulizi zaidi Lebanon
3 Desemba 2024Matangazo
Matukio hayo ya kushambuliana yameyaweka makubaliano ya usitishaji vita yaliyosimamiwa na Marekani katika hali tete, wiki mbili baada ya kuanza kutekelezwa.
Kwa upande mwingine Israel pia imezungumzia kuvunjwa moyo na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani baada ya mataifa hayo kuitaka serikali mjini Tel Aviv ichukue hatua za dharura kuruhusu msaada kuingia Ukanda wa Gaza.
Israel yafanya mashambulizi makubwa nchini Lebanon
Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ziliiandikia barua Israel zikisema hali ya kibinadamu iliyoko Gaza haikubaliki.
Wizara ya mambo ya nje wa Israel imejibu kwa kukanusha kuwa imeweka masharti ya kuzuia msaada kuingia Gaza.