Israel yaapa kujibu shambulizi la Iran la mwishoni mwa juma
19 Aprili 2024Washirika wa Israel wamekuwa wakiitaka kujizuia kufuatia shambulio hilo la Iran ambayo kwa sasa viongozi wa Umoja wa Ulaya wameapa kuongeza mbinyo wa vikwazo dhidi yake wakilenga usafirishaji wake wa ndege zisizo na rubani na makombora kwa washirika wake wa Ukanda wa Gaza, Yemen na Lebanon.
Marekani ambayo nayo iliweka vikwazo ambavyo vimelenga watu binafsi pamoja na wazalishaji wa zana hizo. mashambulizi ya Iran siku ya Jumamosi, yaliashiria mara ya kwanza kwa Tehran kufanya shambulio la kijeshi na la moja kwa moja dhidi ya Israel.
Soma pia:Kwanini Iran na Israel ni maadui?
Mamlaka ya Israel ilisema Iran ilirusha zaidi ya makombora na droni 300 na asilimia 99 ya mashambulizi hayo yalizuiliwa na mifumo ya ulinzi wa anga wakishirikiana na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Jordan.