Israel huenda ikapiga marufuku operesheni za UNRWA
29 Oktoba 2024UNRWA ndilo shirika kuu linalotoa msaada wa kiutu katika Ukanda wa Gaza. Hatua ya Israel huenda ikatishia kazi ya shirika hilo huko Gaza, ikizingatiwa inavitegemea vivuko vya mpakani vya Israel kuingia katika Ukanda huo. Israel inadai kuwa shirika hilo limeingiliwa na mamia ya kile inachoita "magaidi" wa Kipalestina.
Soma pia: Wachunguzi: Israel haina ushahidi dhidi ya UNRWA
Maafisa wa Israel hawajatoa ushahidi wa kuthibitisha madai hao. Mwezi Agosti, UNRWA ilisema wafanyakazi wake saba "huenda walihusika katika mashambulizi ya Oktoba 7." Shirika hilo liliwafuta kazi baada ya mfululizo wa uchunguzi.
Lakini pia lilihoji kuwa ukosoaji wa Israel wa shirika hilo haukuwa kila wakati halali. Nchi za Magharibi ikiwemo Ujerumani zilikuwa zimeonya dhidi ya hatua ya kusitisha operesheni za UNRWAnchini Israel.