Norway, Ireland na Uhispania zatambua Palestina kama dola
22 Mei 2024Matangazo
Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere amesema hakuwezi kuwa na amani Mashariki ya Kati bila kuwepo suluhu ya madola mawili
Ireland nayo kupitia Waziri wake Mkuu Simon Harris imesema imechukua hatua hiyo iliyoitaja ya kihistoria kwa nchi yake na watu wa Paletina, kama njia ya kusaidia kupata suluhu katika mzozo wa Israel na Hamas ulioanza Oktoba 7. Utambuzi rasmi utafanyika tarehe 28 Mei.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel Israel Katz amewaamurumabalozi wa Ireland na Norway kurejea nyumbani mara moja kufuatia mataifa hayo kuitambua Palestina kama dola huru. Kiongozi wa Palestina Mahmood Abbas amekaribisha uamuzi huo na kuyataka mataifa mengine kuchukua hatua kama hiyo.