1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaNiger

IRC: Mamilioni hawana chakula mataifa matatu kanda ya Sahel

7 Mei 2024

Shirika la kimataifa la msaada wa kiutu International Rescue Committee (IRC) limesema idadi ya watu wanaotaabika kutokana na ukosefu "mkubwa" wa chakula kwenye mataifa matatu ya kanda ya Sahel imefikia milioni 7.5.

https://p.dw.com/p/4fZBJ
Niger - Mkulima
Mavuno duni na ukosefu wa usalama ni miongoni mwa vyanzo vya ukosefu wa chakula kwenye kanda ya Sahel.Picha: picture-alliance/EPA/Marcel Mettelsiefen

Shirika hilo limesema kiwango cha ukosefu wa chakula kwenye nchi za Mali, Burkina na Niger kimezidi kupanda ikiwa ni pamoja na visa chungunzima vya utapiamlo.

Kwenye mataifa hayo matatu yaliyo chini ya tawala za kijeshi idadi hiyo ya watu milioni 7.5 imepanda kutoka milioni 5.4 mwaka uliopita.

IRC imetahadharisha hali kama hiyo inaweza pia kusambaa kwenye mataifa mengine ya Cameroon, Chad na Nigeria iwapo hakutakuwa na mavuno ya kutosha ya chakula.