Iraq yajitolea kusimamia juhudi za kumaliza vita Yemen
23 Julai 2023Iraq imejitolea kuwa msuluhishi wa pande zinazozozana nchini Yemen, katika juhudi za kumaliza vita vya muda mrefu. Waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq Fouad Hussein ametoa pendekezo hilo, wakati wa ziara ya waziri wa masuala ya kigeni wa Yemen Ahmed bin Mubarak.Wasaudia wakutana na waasi wa Houthi kutafuta amani Yemen
Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iraq, waliudhibiti mji mkuu Sanaa mwaka 2014, kabla ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia kuingilia kati kuisaidia serikali inayoungwa mkono kimataifa. Kwa sasa mapambano bado yamesitishwa licha ya makubaliano ya kuweka silaha chini kati ya pande zinazozozana yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa kumaliza muda wake tangu mwezi Oktoba mwaka jana.
Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mzozo wa Yemen katika kile Umoja wa Mataifa unachokiita kuwa mgogoro mbaya zaidi wa kiutu kuwahi kutokea duniani.