1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIraq

Marekani yakubaliana na Iraq kuondoa wanajeshi wake

9 Septemba 2024

Iraq na Marekani zimekubaliana juu ya kuondolewa nchini Iraq kwa muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani, awamu kwa awamu lakini bado nchi hizo hazijatia saini makubaliano ya mwisho.

https://p.dw.com/p/4kQi1
Wanajeshi wanaoongozwa na Marekani wakiondoka katika kambi ya Taji ya Iraq
Wanajeshi wa Marekani wakati wa hafla ya kukabidhi kambi ya kijeshi ya Taji iliyokuwa inakaliwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Iraq, kaskazini mwa Baghdad, Iraqi Agosti 23, 2020.Picha: Thaier Al-Sudani/File PhotoU*/REUTERS

Waziri wa ulinzi wa Iraq Thabet al-Abbassi, ameeleza hayo.

Marekani inao wanajeshi wapatao 2,500 nchini Iraq na 900 nchini Syria kama sehemu ya muungano wa kimataifa dhidi ya kundi linaloitwa Dola la Kiislamu, IS.

Pande hizo mbili zimekuwa zinafanya mazungumzo kwa miezi kadhaa juu ya kuondolewa kwa majeshi hayo lakini bado hazijakubaliana juu ya ratiba.

Hata hivyo, Waziri al-Abbassi amesema majeshi hayo yataondoka kwenye kambi za Baghdad na maeneo mengine.

Kwa mujibu wa waziri huyo wa Iraq, waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa muda wa miaka miwili hautatosha kwa majeshi hayo kuondoka Iraq.