1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yathibitisha adhabu ya kifo dhidi ya Jamshid Sharmahd

27 Aprili 2023

Mahakama kuu ya nchini Iran imethibitisha adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya mtu mwenye uraia wa Iran na Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4QbtA
Iran Jamshid Sharmahd im US-Gefangenen-Prozess
Picha: KOOSHA MAHSHID FALAHI/MIZAN NEWS AGENCY/AFP via Getty Images

Mnamo mwezi wa Februari Jamshid Sharmahd alikutwa na hatia ya shambulio la kigaidi na pia hatia ya kushirikiana na mashirika ya ujasusi ya nchi za nje. Hata hivyo bado haijawa wazi iwapo adhabu hiyo itatekelezwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameitaka Iran ipindue hukumu hiyo. Ameeleza kuwa juhudi zote zinafanyika ili kuzuia utekelezaji wa adhabu hiyo dhidi ya raia huyo wa Iran na Ujerumani mwenye umri wa miaka 68.

Soma pia: Ujerumani yakosoa hukumu ya kifo kwa raia wake, Iran

Binti yake ameilaumu serikali ya Ujerumani kwa kutochukua hatua za haraka. Amesema amekuwa anatadharisha juu ya mkasa huo kwa muda mrefu. Sharmahd alikuwa anaishi nchini Marekani kwa miaka mingi hadi alipokamatwa huko Dubai na majasusi wa Iran mnamo mwaka 2020.