Iran yasitisha kumpeleka balozi wake nchini Sweden
2 Julai 2023Waziri huyo wa masuala ya kigeni wa Iran, ametoa taarifa hiyo leo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter akisema kuwa licha ya taratibu zote za kumteua balozi kukamilika, mchakato wa kumpeleka Sweden umesimama kutokana na serikali ya Sweden kuruhusu kuchomwa kwa kitabu hicho kitakatifu cha Quran Jumatano iliyopita. Mwanaume aliyefanya tukio hilo aliyejitambulisha kama mkimbizi kutoka Iraq, tayari ameshafunguliwa mashtaka.
Polisi nchini Sweden yakataa maandamano ya kupinga Koran
Amirabdollahian hakusema ni kwa muda gani Iran imesitisha kupeleka balozi wake Sweden. Licha ya Polisi nchini Sweden kukataa maombi kadhaa ya hivi karibuni ya maandamano ya kupinga Quran, mahakama zimekuwa zikitupilia mbali maamuzi hayo zikidai kuwa kufanya hivyo kunakiuka haki ya uhuru wa kujieleza.