1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yadaiwa kuwafukuza waandishi 6 wa Iran

29 Mei 2024

Iran imesema, Saudi Arabia imewafukuza wafanyakazi sita wa kituo cha televisheni ya taifa ya Iran baada ya kuwashikilia kizuizini kwa takriban wiki moja nchini humo kuelekea ibada ya Hajj.

https://p.dw.com/p/4gQlM
Iran
Kituo cha Televisheni cha Iran kimesema waandishi wake walikwenda Saudi Arabia kuripoti shughuli za ibada ya Hajj.Picha: IRANIAN STATE TV/EPA

Kituo cha Televisheni cha Iran kimesema waandishi wake hao walikwenda Saudi Arabia kuripoti shughuli za ibada ya Hajj.

Saudi Arabia haikutoa tamko lolote la haraka kukiri juu ya kutokea tukio hilo ambalo linashuhudiwa mwaka mmoja baada ya mataifa hayo mawili kufikia makubaliano ya ushirikiano yaliyosimamiwa na China.

Hata hivyo kumekuweko mivutano kwa miongo kadhaa kati ya Saudi Arabia inayotawaliwa na madhehebu ya Sunni na Iran inayoongozwa na Washia kuhusiana na maeneo matakatifu yaliyoko Saudi Arabia na hasa katika kipindi cha kuelekea ibada kubwa kwa Waislamu ya Hajj.Ibada hiyo inatarajiwa mwaka huu kuanza rasmi tarehe 14 mwezi Juni
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW