Iran yasema ripoti ya IAEA haina mashiko
27 Desemba 2023Matangazo
Mkuu wa shirika la Atomiki la Iran Mohammad Eslami amesema hakuna chochote kipya walichokifanya na shughuli zao zinafuata kanuni zilizopo, akiongeza kuwa wanaendelea kuzalisha asilimia 60 ya madini hayo na hakuna kilichoongezeka.
Hopa jana IAEA ilitoa ripoti iliyodai Iran imezidisha kiwango chake cha uzalishaji wa madini hayo kwa kilo 9 zaidi tangu mwishoni mwa mwezi Novemba. Urutubishwaji mkubwa zaidi wa madini ya Urani wa asilimia 90 ndio unaohitajika kutengeneza silaha za nyuklia.