1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema bado ina nia ya kumuua Donald Trump

25 Februari 2023

Jenerali mmoja wa Iran ameonya kuwa nchi yake bado ina nia ya kumuua rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ili kulipiza kisasi kutokana na mauaji ya Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran, jenerali Qasem Soleimani.

https://p.dw.com/p/4NyjP
Iran, Teheran | Demonstration vor der US-Botschaft
Picha: Vahid Salemi/AP/picture alliance

Iran imekuwa ikirejelea kauli yake ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kamanda huyo aliyesimamia operesheni za kigeni, aliyeuwawa kwa shambulio lililofanywa na ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani, katika uwanja wa ndege wa Baghdad mwezi Januari mwaka 2020. 

Rais wa Iran Ebrahim Raisi aapa kisasi kwa mauaji ya jenerali Qassem Soleimani

Brigedia jenerali Amirali Hajizadeh wa jeshi la kimapinduzi la Jamhuri hiyo ya kiislamu, amesema wanatumai watafanikiwa kumuua Trump, pamoja na aliyekuwa Waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo, Jenerali wa zamani wa jeshi la Marekani Kenneth McKenzie na makamanda wengine wa kijeshi waliotoa amri ya kuuwawa kwa Soleimani. 

Marekani na washirika wake wamekuwa na wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran pamoja na Jukumu lake katika kanda ya Mashariki ya kati.