1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yalalamikia rasmi kukamatwa raia wake wawili

22 Desemba 2024

Iran imetoa malalamiko rasmi kupinga hatua ya kukamatwa raia wake wawili nchini Italia na Marekani, wakituhumiwa kuhamisha teknolojia nyeti ya Marekani kwa Iran.Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya ndani ya Iran.

https://p.dw.com/p/4oTrD
Marekani na Iran
Bendera za Iran na MarekaniPicha: Dado Ruvic/REUTERS

Iran imetoa malalamiko rasmi kupinga hatua ya kukamatwa raia wake wawili nchini Italia na Marekani, wakituhumiwa kuhamisha teknolojia nyeti ya Marekani kwa Iran.Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya ndani ya Iran. 

Waendesha mashtaka wa Marekani walifungua mashtaka dhidi ya Mahdi MohammadSadeghi na Mohammad Abedininajafabadi kwa tuhuma kwamba walishirikiana kusafirisha vifaa vya kimamboleo vya kielekroniki kutoka Marekani hadi Iran kinyume na vikwazo na sheria ya Marekani ya udhibiti wa kusafirisha vifaa. 

Soma zaidi. Ujumbe wa Marekani wawasili Damascus kwa mazungumzo

Taarifa ya idara ya sheria ya Marekani pia imesema kwamba teknolojia hiyo iliyochukuliwa kinyume cha sheria ilitumika mwezi Januari katika shambulio la droni lililouwa wanajeshi watatu wa Marekani nchini Jordan. Iran hata hivyo imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulio hilo,ikisema tuhuma dhidi yake hazina msingi.