1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Narges Mohammed anyimwa matibabu kwa kutovalia hijabu

2 Novemba 2023

Mamlaka Iran imemzuia mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2023 Narges Mohammadi kuhamishiwa hospitali nyengine kwa ajili ya matibabu ya dharura, kufuatia hatua yake ya kukataa kuvaa hijabu.

https://p.dw.com/p/4YKSk
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2023 Narges Mohammadi
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2023 Narges MohammadiPicha: Mohammadi family archive photos/Handout via REUTERS

Haya yamesemwa na familia ya mshindi huyo wa tuzo ya Nobel. Katika taarifa, familia hiyo imesema mamlaka za magereza nchini Iran zimekataa kumhamisha Mohammadi katika hospitali nje ya mji wa Evin licha ya kuwa anaugua maradhi ya moyo na mapafu.

Familia hiyo sasa inasema afya na maisha yake viko hatarini.

Mohammadi ametangaza kwamba hatovaa hijab kwa hali yoyote ile.

Wanawake nchini Iran wamekuwa wakikabiliwa na changamoto inayotokana na sheria ngumu za Kiislamu nchini humo

Mwanaharakati huyo mkongwe wa haki za binadamu mwenye umri wa miaka 51, ambaye kwa sasa anashikiliwa katika jela ya Evin mjini Tehran, alitunukiwa tuzo ya Nobel mwezi Oktoba kwa "mapambano yake dhidi ya ukandamizaji wa wanawake nchini Iran." 

Uvaaji wa hijabu ni lazima kwa wanawake Iran.