1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Iran yakaribisha wito wa marekani kuunga mkono amani Yemen.

5 Aprili 2023

Iran Jumatano imepongeza wito wa Marekani kusaidia kumaliza mgogoro nchini Yemen kwa kuunga mkono mchakato wa amani, mwaka mmoja baada ya makubaliano ya amani yalioongozwa na Umoja wa Mataifa kupunguza mapigano.

https://p.dw.com/p/4PjFB
Jemen Sanaa | Saudi-geführte Luftangriffe auf Häuser
Picha: Hani Mohammed/AP Photo/picture alliance

Juhudi za kidiplomasia kutatua mgogoro wa Yemen zimeongezeka tangu mshirika mkuu wa serikali ya Yemen, Saudi Arabia, kutia Saini mkataba uliosimamiwa na China kuimarisha  uhusiano na Iran mwezi uliopita.

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa Yemen Timothy Lenderking amesema Jumanne kwamba nchi hiyo ingependa kuona Wairani wakiunga mkono mchakato huo wa kisiasa wanaotumaini utakamilishwa.

Iran yasema imekuwa ikitaka amani kudumishwa

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani alielezea wito wa mjumbe huyo kuwa wa kufurahisha na kusisitiza kuwa Iran imekuwa ikipigania  mchakato wa amani tangu kuanza kwa vita.

Maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa makubaliano

Jumapili iliadhimisha mwaka wa kwanza wa mkataba wa amani uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa kati ya serikali ya Yemen na waasi wanaoungwa mkono na Iran wanaothibiti mji mkuu Sanaa na maeneo mengi ya Kaskazini.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Hans Grundberg, aliutaja kuwa wakati wa matumaini kwasababu mkataba huo ulikuwa bado unatekelezwa pakubwa licha ya muda wake kukamilika mwezi Oktoba.

Rais wa Marekani aliahidi kumaliza vita hivyo

Rais wa Marekani Joe Biden alichukuwa hatamu za uongozi kwa kuahidi kutoa kipaombele katika kumaliza vita hivyo vikali baada ya mtangulizi wake Donald Trump kuunga mkono muingilio wa kijeshi ulioongozwa na Saudi Arabia kwa kuiunga mkono serikali.

Takriban muongo mmoja wa vita umegharimu maisha ya maelfu ya watu aidha moja kwa moja ama kwa njia zisizo za moja kwa moja na kuchochea kile Umoja wa Mataifa ulichokitaja kuwa mzozo mbaya zaidi kwa kibinadamu.