1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yafanya uchaguzi wa bunge

1 Machi 2024

Iran ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa bunge siku ya Ijumaa tangu maandamano makubwa ya mwaka 2022 yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini aliyekufa mikononi mwa polisi ya maadili alikoshikwa kwa kutovaa hijabu.

https://p.dw.com/p/4d4Ee
Masanduku ya kura kwenye uchaguzi wa Iran.
Masanduku ya kura kwenye uchaguzi wa Iran.Picha: Arne Immanuel Bänsch/dpa/picture alliance

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei mwenye umri wa miaka 84, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupiga kura zao katika uchaguzi huo ambao wabunge na wataalamu wapya wa bunge la taifa wanachaguliwa.

Soma zaidi: Iran yajiandaa kwa uchaguzi unaohodhiwa na wahafidhina

Kiongozi huyo aliwahimiza watu kupiga kura haraka iwezekanavyo katika uchaguzi huo, akisema marafiki na maadui wa Iran walikuwa wakitazama watu waliojitokeza kupiga kura.

Wagombea 15,000 wanawania viti 290 vya bunge hilo.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kuanza kutoka siku moja baadaye.