SiasaAsia
Iran wapigakura duru ya pili kumchaguwa rais
5 Julai 2024Matangazo
Uchaguzi wa leo ni baina ya mwanamageuzi Masoud Pezekshian na mhafidhina Saeed Jalili.
Kwenye duru ya kwanza wiki iliyopita, Pezekshian alipata asilimia 42, huku Jalili akimfuatia kwa asilimia 39 ya kura.
Soma zaidi:
Juzi Jumatano, kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, aliwatolea wito wananchi kujitokeza kwa wingi vituoni, baada ya duru ya kwanza kushuhudia asilimia 41 tu ya wapigakura halali.
Pezekshian, ambaye ni daktari bingwa wa moyo na pia mbunge wa mji wa kaskazini magharibi wa Tabriz tangu mwaka 2008, anaungwa mkono na marais wawili wa zamani, Mohammad Khatami na Hassan Rouhani, wote wanamageuzi.