Iran: Waandamanaji waadhimisha mwaka mmoja wa ukandamizaji
30 Septemba 2023Vidio zilizochapishwa kwenye mtandao wa X na shirika la kutetea haki za binadamu la Iran - IHR, zimeonyesha waandamanaji wakikabiliana na vikosi vya usalama mjini Zahedan, mji mkuu wa mkoa wa kusini mashariki wa Sistan-Baluchistan.
Mashirika ya haki za binadamu ya IHR na Hal Vash yamesema takriban watu 23 wamejeruhiwa. Shirika la habari la Reuters hata hivyo halikuweza kuthibitisha ripoti za majeruhi hao au uhalisia wa vidio zilizochapishwa mtandaoni.
Shirika la Amnesty International limeeleza kuwa, mnamo Septemba 30 mwaka jana, vikosi vya usalama vya Iran viliua takriban watu 66.
Mamlaka iliwatuhumu waandamanaji, waliokasirishwa na madai ya kubakwa kwa msichana kutoka jamii ya walio wachache ya Baluch na kamanda wa polisi, kwa kuchochea ghasia hizo.