Kwa mwaka uliopita Iran imewanyonga watu 834
5 Machi 2024Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na shirika la haki za binadamu lenye makao yake makuu Norway na jingine la mjini Paris. Mashirika hayo yamesema idadi ya watu walionyongwa, kwa Iran kutekeleza adhabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni, iliongezeka kwa asilimia 43, mwaka 2022. Mashirika hayo yameishutumu Iran kwa kutumia hukumu ya kifo kueneza hofu katika jamii katikati mwa maandamano yaliyochochewa na kifo cha msichana Mahsa Amini Septemba mwaka 2022. Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, adhabu ya kifo pia ilitekelezwa katika mashitaka mengine ikiwa ni pamoja na kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya.