IOM: Watu 25 wafariki baada ya kupindukia kwa boti Comoros
5 Novemba 2024Katika taarifa, IOM imesema boti hilo lilizama Ijumaa jioni kati ya kisiwa cha Comoro cha Anjouan na kile cha Ufaransa cha Mayotte kwenye njia ya wahamiaji inayotumiwa mara kwa mara ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha katika muda wa miaka mingi.
Wahanga wa ajali ni raia wa mataifa tofauti
Wavuvi waliwaokoa manusura watano Jumamosi asubuhi. Manusura hao walisema boti hiyo ilikuwa imebeba takriban watu 30 wa mataifa tofauti, wakiwemo wanawake saba na watoto sita wadogo.
Comoro yakataa kuwapokea wahamiaji wa Mayotte
Taarifa ya IOM ilinukuu ripoti kutoka kwa baraza la seneti la Ufaransa lililokadiria kuwa kati ya watu 7,000 na 10,000 walipoteza maisha wakijaribu kuvuka kutoka Comoro kwenda Mayotte kati ya mwaka 1995 na 2012, lakini ikasema huenda idadi hiyo ikawa juu zaidi.