Inter Milan imeichapa AC Milan 2-0
11 Mei 2023Kwa hatiua hiyo sasa Inter wamejiweka katika nafasi ya katika matarajio ya mechi ya duru ya pili ya Jumanne ijayo, ikitawajwa kuwa "derby" kubwa zaidi kwa miongo kadhaa, kwa Milan, ambapo shukrani za dhati zikiwaangukia wachezaji Edin Dzeko na Henrikh Mkhitaryan kwa mashambulizi ya mapema kabisa.
Kikosi cha Simone Inzaghi kilikuwa kinastahili ushindi kwenye uwanja wa San Siro baada ya kutengeneza nafasi nyingi na kuwaruhusu Milan kunusa mbele ya lango.
Nafasi nyingi za ushindi kwa Inter Milan
Inter Milan wangeweza kushinda kwa tofauti kubwa zaidi huku Hakan Calhanoglu akipiga shuti lililotoka nje ya lango na Dzeko akapoteza nafasi kubwa mapema kipindi cha pili, lakini bado wanapewa nafasi kubwa ya kutinga fainali ya mchuano huo mikuu wa ligi ya mbaingwa ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu washinde miaka 13 iliyopita.
Mshindi wa mechi hiyo atamenyana na mabingwa Real Madrid au Manchester City katika mnyukani wa lJuni 10 mjini Istanbul.
Huko Afrika Mashariki, Klabu ya Yanga ya Tanzania imeibuka na usindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kutanguliza mguu mmoja katika fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya kiungo Stephane Aziz Ki, dakika ya 64 na Winga wao Benard Morrison dakika ya 90 na sekunde kadhaa.
Soma zaidi:Mahasimu wa Milan kukutana nusu fainali ya Champions League
Kutokana na matokeo hayo yanga inahitaji ushindi au sare katika mechi ya marudino itakayochezwa Afrika Kusini Mei 17 mwaka huu ili kutinga fainali. Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kufika nusu fainali ya michuano ya CAF.
Chanzo: AFP