1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India kukabiliwa na wimbi jingine la joto kali kwa wiki 3

Sylvia Mwehozi
17 Mei 2024

Idara ya hali ya hewa nchini India imeonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la pili la joto kali katika muda wa wiki tatu, ikiwemo maeneo ambayo mamilioni ya watu wanatazamiwa kupiga kura katika uchaguzi wa wiki sita.

https://p.dw.com/p/4g0t3
India-Joto kali
Joto kali IndiaPicha: Sudipta Das/NurPhoto/NurPhoto/picture alliance

Idara ya hali ya hewa nchini India imeonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la pili la joto kalikatika muda wa wiki tatu, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo mamilioni ya watu wanatazamiwa kupiga kura katika uchaguzi wa wiki sita.

Idara ya hali ya Hewa ya India imeelezea "wasiwasi wa kiafya wa wastani" kwa watoto wachanga, wazee na wale walio na magonjwa sugu, na kuwashauri wakaazi wa majimbo hayo kuepuka kukaa kwenye maeneo ya joto. Mji mkuu waNew Delhi unatarajiwa kuwa na viwango vya juu vya joto vya 45C mwishoni mwa juma, kulingana na utabiri.

India-Joto kali
Wimbi la joto kali IndiaPicha: Subrata Goswami/DW

Majimbo ya Uttar Pradesh, Bengal Magharibi, Maharashtra na Jharkhand, ambayo yote yatapiga kura siku ya Jumatatu, yanatarajia hali ya "wastani" ya joto ikiwa ni pamoja na nyuzi joto 40 C.

Katika mji wa Mathura, ulio karibu na New Delhi, kiwango cha nyuzi joto kilivuka 41C siku ya upigaji kuramwishoni mwa mwezi Aprili, huku takwimu za tume ya uchaguzi zikionyesha kupungua kwa wapiga kura waliojitokeza kwa karibu pointi tisa ukilinganisha na miaka mitano iliyopita.

Tume ya uchaguzi ya India ilisema mwezi uliopita ilikuwa imeunda jopokazi la kukagua athari za joto kabla ya kila duru ya upigaji kura.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliwataka wapiga kura mwezi huu kunywa "maji mengi iwezekanavyo" siku ya kupiga kura katika jimbo lake la nyumbani la Gujarat.

Joto kali India
Tunajaribu kupunguza joto kaliPicha: ARUN SANKAR/AFP/Getty Images

India imekuwa ikikabiliwa na viwango vya joto kali wakati wa kiangazi lakini utafiti wa kisayansi umegundua kwamba mabadiliko ya Tabianchi yamesababisha msimu wa joto kuwa marefu, wa mara kwa mara na mkali zaidi katika bara la Asia na duniani kote.Indian yarejea kwenye uchaguzi katikati ya kitisho cha joto

Mamilioni ya watu katika maeneo ya Kusini-mashariki mwa Asia wamekabiliwa na wimbi la joto la muda mrefu mwezi uliopita ambalo lilisababisha kufungwa kwa shule nchini Ufilipino na Bangladesh.

Dhoruba kali pia zimeshuhudiwa katika nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu wa kifedha wa Mumbai, ambapo upepo mkali uliangusha bango kubwa ambalo liliua watu 16 na kuwaacha makumi ya wengine wamenaswa chini ya mabaki.

Takriban watu 11 waliuawa katika milipuko ya radi wakati wa mvua huko West Bengal wiki hii.