1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF yaidhinisha kupunguza gharama za kukopa kwa 36%

12 Oktoba 2024

Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, imeidhinisha mageuzi ambayo yatashusha gharama za kukopa kwa asilimia 36, sawa na dola bilioni 1.2 kwa mwaka.

https://p.dw.com/p/4li1m
Mkurugenzi Mkuu wa IMF,  Kristalina Georgieva.
Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva.Picha: DW

Mageuzi hayo pia yanaziondoshea nchi zenye madeni makubwa masharti ya kulipia zaidi ili ziweze kukopeshwa tena.

Mageuzi hayo yaliyotangazwa jana Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva, yanajumuisha marekebisho kwenye riba ya utunzaji wa deni yanayofanywa na mataifa yenye madeni makubwa, kama vile Ukraine na Argentina.

Soma zaidi: IMF yapokea maombi ya kuitathmini Kenya

IMF imesema utekelezaji wa mageuzi hayo utakaoanza Novemba Mosi utapandisha ukomo wa kukopa kwa mataifa wanachama wanaolipia riba ya utunzaji madeni.

Nchi nane zilizoendelewa sharti la kulipia zaidi ili zikopeshwe tena ni Benin, Ivory Coast, Gabon, Georgia, Moldova, Senegal, Sri Lanka, na Suriname.