IMF, Benki ya Dunia, zafanya mikutano barani Afrika
10 Oktoba 2023Georgieva amesema haya Jumatatu (09.10.2023) wakati wa ufunguzi wa mikutano ya kwanza ya shirika hilo la IMF na Benki ya Dunia inayofanyika barani Afrika baada ya miaka 50. Katika mkutano na wanachama wa mashirika ya kiraia, Georgieva amesema kufanywa tena kwa mikutano hiyo barani Afrika ni kiashiria muhimu sana.
Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto sawa na za miaka 50 iliyopita
Georgieva ameongeza kuwa bara Afrika linakabiliana na changamoto sawa na zilizokuwa miaka 50 iliyopita, zinazojumuisha mfumuko wa bei na machafuko ya kisiasa katika maeneo mengi.
Mataifa mengi yanakabwa na mzigo wa madeni
Georgieva pia amesema kuwa nchi nyingi zinakabiliwa na mzigo wa madeni unaoweza kuzisambaratisha na akaelezea matumaini kwamba mikutano hiyo itasaidia kujenga imani kati ya mataifa.
Georgieva ameongeza kuwa shirika la IMF na Benki ya Dunia zinahitaji uwezo zaidi kuzisaidia nchi zinazohitaji msaada ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba sifuri kwa kiwango kikubwa.