MigogoroUjerumani
MOSCOW: Scholz yupo sahihi kutaka uchunguzi wa Nord Stream
9 Septemba 2024Matangazo
Urusi imesema hayo, katikati ya kile ilichoita majaribio ya baadhi ya nchi za Magharibi kunyamazisha kile kilichotokea.
Scholz alisema katika mahojiano na televisheni ya Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba Ujerumani itahakikisha kuwa hakuna kitu kitakachofichwa katika uchunguzi huo na kwamba waliohusika na hujuma hiyo wataadhibiwa.
Urusi imelalamika mara kwa mara kwamba Ujerumani haijafanya vya kutosha kuchunguza hujuma hizo zilizosababisha mabomba mawili ya Nord Stream kupasuka. Mabomba hayo yalijengwa kusafirisha gesi ya Urusi hadi Ulaya chini ya Bahari ya Baltic.
Mwezi uliopita waendesha mashtaka wa Ujerumani walitoa hati ya kuwezesha kukamatwa kwa mkufunzi wa kupiga mbizi wa Ukraine nchini Poland kuhusiana na mashambulizi hayo.