1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika Kusini

Vifo vya mkasa wa kuporomoka jengo Afrika Kusini vyafikia 24

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo la gorofa nchini Afrika Kusini imeongezeka na kufikia watu 24.

https://p.dw.com/p/4fo2s
Afrika Kusini | Mkasa wa kuporomoka kwa jengo
Juhudi za kuwatafuta watu waliokamwa kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka Afrika Kusini zikiendelea.Picha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Watu wengine 28 bado hawajapatikana. Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu na maafisa wa serikali, wiki moja baada ya maafa hayo.

Miili mingine minne ilitolewa kwenye vifusi usiku wa kuamkia leo, katika mji wa kitalii wa George. Vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta manusura, tangu lilipo-poromoka jengo la ghorofa tano, lililokuwa likijengwa, Jumatatu iliyopita.

Watu themanini na moja, wengi wao wakiwa wajenzi, walikuwa kwenye eneo hilo wakati wa tukio. Watu 29 tayari wameokolewa. Ikiwa ni pamoja na mwanamume aliyeokolewa akiwa hai baada ya saa 116 chini ya vifusi.

Kikosi cha uokoaji kinaendelea na juhudi zake, lakini uwezekano wa kuwapata manusura ni mdogo. Jamaa wa waathiriwa wameelezea kukerwa na kasi ndogo katika mchakato wa kutambua maiti. Sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo, haija bainishwa, na uchunguzi unaendelea.