JamiiDjibouti
Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti Djibouti imepanda
25 Aprili 2024Matangazo
Ajali hiyo ya Jumatatu ni ya pili mbaya ya baharini katika muda wa wiki mbili katika nchi hiyo iliyoko kwenye kile kinachojulikana kama Njia ya Uhamiaji ya Mashariki kutoka Afrika hadi Rasi ya Arabia.
Katika taarifa hapo jana jioni, IOM imesema kuwa takriban watu 24, walifariki dunia na wengine 20 hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji 77 wakiwemo watoto, kuzama karibu na mji wa Obock
IOM imesema kuwa manusura 33 wanaendelea kupata huduma katika kituo cha IOM mjini humo Obock na kwamba maafisa wa eneo hilo wanaendelea kuwaendeleza juhudi za uokoaji kwa matumaini ya kuwapata manusura zaidi.