Idadi ya wagonjwa wa homa ya mafua yaongezeka Uingereza
9 Januari 2025Matangazo
Takwimu kutoka huduma ya kitaifa ya afya nchini humo NHS zinaonyesha kwamba, kulikuwepo wastani wa wagonjwa 5,408 wa homa ya mafua waliolazwa hospitali kila siku wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 256 waliokuwa kwenye huduma za dharura.
Takwimu hii ni ongezeko la asilimia 21 kutoka wagonjwa 4,469 wiki iliyopita ambapo wagonjwa 211 walihitaji huduma za dharura.
Pia idadi hiyo ni karibu mara tano ya idadi ya wagonjwa waliolazwa mnamo Desemba mosi, wakati huo kulikuwepo wagonjwa 1,098.