1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Idadi ya vifo kutokana na mafuruko Myanmar yaongezeka

Josephat Charo
17 Septemba 2024

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko makubwa nchini Myanmar kufuatia kimbunga Yagi imeongezeka maradufu hadi kufikia 226. Taarifa hii imeripotiwa na chombo cha habari cha serikali ya Myanmar.

https://p.dw.com/p/4kiIN
 Myanmar | Ng#ombe na watu wakichukuliwa na mafuriko.
Mafuriko yameathiri maeneo makubwa ikiwemo maeneo ya wakulima na wafugaji.Picha: Sai Aung Main/AFP/Getty Images

Kimbunga Yagi kilipiga maeneo ya kaskazini mwa Vietnam, Laos, Thailand na Myanmar zaidi ya wiki moja iliyopita huku kikiandamana na upepo mkali na mvua kubwa na kusababisha mafuriko na maporomoko ya tope ambayo yamesababisha vifo zaidi ya 500 kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Soma pia:Watu 18 wafariki dunia kutokana na mafuriko barani Ulaya

 Wakala wa kushughulikia majanga wa Afisi ya Umoja wa Mataifa ya utatibu wa misaada ya kibinadamu UNOCHA, umesema watu wanaokadiriwa kufikia 631,000 wameathiriwa na mafuriko kote nchini Myanmar.

UNOCHA imesema chakula, maji ya kunywa na nguo vinahitajika kwa dharura na imetahadharisha kwamba barabara zilizofungwa na madaraja yaliyohabiriwa yanakwamisha kwa kiwango kikubwa juhudi za utoaji wa misaada.