JangaAfrika
Idadi ya vifo kutokakana na mafuriko Somalia yakaribia 100
24 Novemba 2023Matangazo
Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na Baraza la Mawaziri la nchi hiyo ambalo limesema idadi kamili sasa imefikia vifo 96.
Mapema mwezi huu, serikali mjini Mogadishu ilitangaza hali ya dharura kutokana na mafuriko hayo yaliyopelekea takriban watu 700,000 kuyahama makazi yao huku mashamba na miundombinu kadhaa vikisombwa na maji.
Soma pia:Wasiwasi wa mafuriko watanda Sudan kufuatia shambulizi katika bwawa
Eneo la Pembe ya Afrika linakumbwa na mvua kubwa za El Nino na ambazo zinatarajiwa kudumu eneo hilo hadi angalau mwezi Aprili mwakani.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi huku makumi ya watu wakiwa tayari wamepoteza pia maisha katika mataifa mengine kama Kenya na Ethiopia.