1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Idadi ya vifo Gaza yafikia yapindukia elfu arobaini

22 Agosti 2024

Watu 40,265 wameuawa na wengine 93,144 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4jnWn
Mzozo wa Mashariki ya Kati | Shambulio la Beit Lahia
Wapalestina wakiondoa vifusi kwenye eneo la shambulizi la Israel kwenye nyumba moja, katikati mwa mzozo kati ya Israel na Hamas, huko Beit Lahia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Agosti 22, 2024.Picha: Mahmoud Issa/REUTERS

Wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la Hamas imesema leo kuwa watu 40,265 wameuawa katika ukanda wa Gaza katika muda wa zaidi ya miezi kumi ya vita kati ya Hamas na Israel.

Idadi hiyo ya vifo inajumuisha watu 42 waliouawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Wizara hiyo ya afya imeorodhesha watu 93,144 waliojeruhiwa katika ukanda huo wa Gaza tangu kuzuka kwa vita hivyo.

Israel yazidisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza

Soma pia:Jeshi la Israel lasonga mbele maeneo ya kati na kusini mwa Gaza

Takwimu hizo zimetolewa wakati Rais wa Marekani Joe Biden akimshinikiza Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu juu ya umuhimu wa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka.

Mazungumzo ya miezi kadhaa ya kusaka makubaliano ya kusitisha mapigano yamefanyika japo kumekuwa na ugumu wa kufikia makubaliano kutokana na masharti yanayotolewa na Israel na Hamas.