1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliouwawa kwa mashambulizi ya Al-shabaab wafikia watu 37

4 Agosti 2024

Idadi ya watu waliouwawa katika mashambulizi katika ufukwe wa pwani ya mji mkuu Mogadishu nchini Somalia imefikia watu 37.

https://p.dw.com/p/4j5c6
Shambulizi la kigaidi la Somalia kwenye ufuo wa Mogadishu
Watu wakiwaa wameubeba mwili wa mwanamke ambaye hakufahamika jina lake aliyeuawa katika ufukwe wa Lido mjini Mogadishu, Somalia Agosti 3, 2024.Picha: Feisal Omar/REUTERS

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa  maafisa wa Somalia. Katika mashambulizi hayo yaliyoanza kufanywa Ijumaa usiku, mwanamgambo wa kundi la Al-Shabaab alijilipua kwa bomu na kisha wabeba silaha wengine walishambulia eneo hilo.

Majeruhi11 wa tukio hilo wako mahututi na wengine  64 wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali kutokana na mkasa huo. Msemaji wa Polisi Abdifatah Adan Hassan amesema kundi la Al-Shabaab halikulenga maafisa wa serikali na wanajeshi pekee bali pia raia wa kawaida.

Wanamgambo hao wenye itikadi kali na wenye mfungamano na kundi la Al-Qaeda wamekuwa wakifanya uasi dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 17.