1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

ICRC yahimiza pande hasimu Mashariki ya Kati kutolenga raia

25 Septemba 2024

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imetoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo wa Mashariki ya Kati kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya wahanga nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4l4ho
Shambulizi la Israel Lebanon
Shambulizi la Israel LebanonPicha: Mahmoud Zayyat/AFP/Getty Images

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imetoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo wa Mashariki ya Kati kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya wahanga wa kiraia nchini Lebanon.

ICRC imesema leo mjini Geneva kwamba sheria ya kimataifa ya kibinadamu iliweka wazi kwamba uangalifu lazima uzingatiwe wakati wote ili kuwalinda raia na mali yao wakati wa operesheni za kijeshi na kutofautisha kati ya mali ya raia na shabaha za kijeshi.

Msemaji wa ICRC Christian Cardon amesema idadi kubwa ya raia bila shaka itaathirika zaidi  ikiwa mzozo utaongezeka.

ICRC inafanya kazi katika migogoro ya kimataifa kudumisha na kuimarisha sheria za kimataifa za kibinadamu, na inazingatia mikataba minne ya Geneva.

ICRC inashirikiana na Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu kwa kutoa msaada kwa waliojeruhiwa na waliopoteza makazi kama vile vifaa vya matibabu kwa hospitali, pamoja na chakula, bidhaa za nyumbani na pesa taslimu kwa wakazi.