1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ yaiamuru Israel kusitisha mashambulizi Rafah

24 Mei 2024

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa imeiamuru Israel kusitisha "mara moja" mashambulizi yake ya kijeshi kwenye mji wa Rafah ulio kusini mwa Ukanda wa Gaza, ikisema hali ya kibinaadamu huko ni janga.

https://p.dw.com/p/4gFfb
Majaji wa Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ.
Majaji wa Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ.Picha: Robin van Lonkhuijsen/ANP/AFP/Getty Images

Uamuzi huo ulisomwa na Jaji Nawaf Salam kwenye makao makuu ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ) mjini The Hague, kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa na Afrika ya Kusini.

Afrika Kusini ilitilia uzito maombi yake hayo kwa kuhoji kwamba hatua za awali za mahakama hiyo kuhusiana na suala la vita vya Gaza zilikuwa hazitoshi.

Soma zaidi: Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza

Licha ya maamuzi ya mahakama hayo kuwa na nguvu za kisheria, lakini haina uwezo wa kulazimisha utekelezwaji wake.

Hata hivyo, inaweza kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuyafanyia kazi.