ICJ kutolea uamuzi kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel
24 Mei 2024Uamuzi huo uliotarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa (24 Mei) mjini The Hague unahusu uwezekano wa kuagiza kuondolewa mara moja kwa jeshi la Israel kutoka mji wa wa Rafah ulio kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza
Rais wa mahakama hiyo, Nawaf Salam, ambaye ni mwanasheria kutoka Lebanon, ndiye aliyetarajiwa kuusoma uamuzi huo.
Afrika Kusini ililitetea shauri lake mbele ya ICJ kwa hoja kwamba hatua za awali za mahakama hiyo kuhusiana na vita vya Gaza hazikuwa zikitosha.
Soma zaidi: ICJ kuamua juu ya kuondoka kwa vikosi vya Israel mjini Rafah
Israel imekanusha madai yote dhidi yake, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitumia suala la haki ya nchi yake kujilinda katika kujibu mashambulizi ya wanamgambo wa Kipalestina dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7.