1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ kuamua hatima ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel

26 Januari 2024

Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ) inatarajiwa hivi leo kuamua hatima ya kesi ya Afrika Kusini ambayo iliishitaki Israel kwa tuhuma mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bhIx
The Hague, Uholanzi, ICJ
Jopo la wanasheria kwenye Mahakama ya Kimaitaifa ya Haki (ICJ) mjini The Hague, Uholanzi.Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Uamuzi wa leo (Januari 26) ICJ ni sehemu ya kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini inayodai kuwa Israel inafanya mauaji ya halaiki katika vita vyake na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Nchi zote mbili zilitoa ushahidi wakati kesi hiyo ilipofunguliwa yapata wiki mbili zilizopita, ambapo Israel ilikanusha vikali madai ya kufanya mauaji ya halaiki.

Mahakama hiyo inaweza kuiamuru Israel kusitisha mapigano huko Gaza.

Soma zaidi: Viongozi wa Kiarabu wana chaguo lipi katika mzozo wa Gaza?

Japo haina nguvu za kusimamia utekelezwaji wa agizo hilo, lakini kama ukitolewa huo utakuwa uamuzi wenye umuhimu mkubwa kisiasa.

Siku moja kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Israel ilionesha imani kuwa ICJ ingeitupilia mbali kesi ya Afrika Kusini.

Kwa upande mwengine, Hamas ilisema itaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo iwapo tu Israel itatii uamuzi huo.