1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA yasaka suluhu kuhusu kinu cha nyukilia cha Zaporizhzhia

Hawa Bihoga
30 Machi 2023

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Atomiki, IAEA, Rafael Grossi amesema anaendelea kufanyiakazi mpango wa maelewano wa usalama katika kinu cha Zaporizhzhia Ukraine, kinachodhibitiwa na Moscow

https://p.dw.com/p/4PUL1
Ukraine Saporischschja | Präsident Wolodymyr Selenskyj & UN-Atomenergiechef Rafael Grossi
Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Grossi ameonya pia juu ya kuongezeka kwa shughuli za kijeshi karibu na mtambo huo.

Wakati wa ziara hiyo ya nadra katika kinu hicho, kikubwa zaidi barani Ulaya, Grossi amesema lazima kuwe na makubaliano ya kikanuni pamoja na maafikiano kati ya Moscow na Kyiv ya kutoshambulia mtambo huo.

IAEA yaonya juu ya shughuli za kijeshi kwenye mtambo wa nyuklia

Kyiv na Moscow zimeshutumiana kwa kushambulia mtambo huo, na hivyo kuongeza hofu ya maafa. Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa kuondolewa kwa vikosi vyote vya kijeshi karibu na eneo hilo la kimkakati.