Huduma ya Intaneti yazimwa Senegal
13 Februari 2024Matangazo
Wizara ya mawasiliano ya nchi hiyo imetangaza kuwa huduma ya intaneti inasitishwa kwa sababu mitandao ya kijamii inatumika kusambaza ujumbe wa chuki ambao tayari umechochea maandamano ya vurugu.
Kwa siku kadhaa sasa Senegal imekumbwa na wimbi la maandamano yaliyochochewa na uamuzi wa Rais Macky Sall la kuuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa Februari 25, katika wakati uongozi wake mihula miwili unaelekea kufikia mwisho.
Umoja wa Mataifa umesema hii leo kwamba unatiwa wasiwasi na mivutano inayoshuhudiwa nchini humo na kuitolea mwito serikali ya Sall kuulinda utamaduni wa miongo mingi wa Senegal wa kuheshimu demokrasia na haki za binadamu.